Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya polisi eneo la Pwani imewatahadharisha wafanyibiashara wa maduka ya rahani eneo la Kisauni dhidi ya kumiliki mali ya wizi.

OCPD katika eneo hilo Richard Ngatia amesema kuwa wataanzisha oparesheni katika maduka hayo ili kutambua jinsi wafanyabiashara hao walivyopata mali hiyo kwani baadhi ya vyombo au mali hiyo niya wizi.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kina mama waliokuwa wametoka sokoni kuporwa bidhaa walizokuwa wamezibeba ndani ya mifuko aina ya gunia na vijana wadogo waliokuwa wamebeba silaha ikiwemo panga.

Ngatia aidha amesema kuwa kila mfanyibiashara atalazimika kutoa risiti ya bidhaa anazomiliki katika duka lake huku wale wanaozungusha bidhaa katika makazi wakilalamika kutaja sehemu wanazotoa bidhaa hizo na kasha kuonyesha vitambulisho vyaa kitaifa.

Ngatia pia amewataka wazazi kuchunguza tabia za wanawao kila wanapotoka na kuingia nyumbani, kwani kumekuwa na malalamishi kutoka kwa wakazi wa eneo hilo kuwa vijana wengi wanajihusisha katika vitendo potovu vikiwemo, wizi na hata kujiunga na kundi la wakali kwanza linalowahangaisha wakazi wa Kisauni na Mishomoroni.

Ngatia amesema haya baada ya kunasa vyombo vinavyoaminika kuwa vya uwizi katika duka moja la rehani katika eneo hilo.