Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi Kibera walinufaika kutokana na tamasha ya kutafuta talanta miongoni mwa vijana.

Kampuni mbalimbali ikiwemo ile ya mawasiliano ya airtel, zilijumuika katika uwanja wa Kamukunji mtaani Kibera kwenye tamasha hiyo.

Tamasha hiyo iliyoandaliwa chini ya mradi wa Human Needs Project, iliyoanza mapema siku ya Jumamosi, ililenga kuwatambulisha vijana wenye vipaji vya kuimba miongoni mwa wakazi wa Kibera na hata kwenye ulimwengu wa muziki.

Meneja mkuu wa mradi wa Human Needs Project Bi Juliet Mbonne, alisema tamasha hizo zilianza ramsi katika mtaa huo kwa kuwa vijana wengi kutoka mtaa wa Kibera wamekuwa wabunifu ila hukosa nafasi ya kujitambulisha kwa wapenzi wa muziki.