Msanii Nyota Ndogo kutoka Mombasa amelalamika kuhusu jinsi picha yake ilivyotumiwa na matapeli kuwalaghai watu.
Nyota huyo aliyetamba na vibao kama Watu na Viatu, Nibebe na Natafuta, ameonyesha kughadhabishwa na matumizi mabaya ya picha yake akiwa na bwanake kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wa instagramu.
“Wapenzi wangu nimepigiwa simu kujulishwa kuwa kuna mtu flani Uganda anatumia picha yangu kutapeli watu bila mimi kufahamu. Watu wamekuwa wakimtumia hela kwa sababu za kutafutiwa mke au mume mzungu,” alisema Nyota Ndogo.
Nyota ndogo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdallah alifunga pingu za maisha na raia wa Denmark Bw Henning Nielson, wiki chache ziliopita.
Picha hio imetumiwa kwa nia ya kuwahujumu watu wanaotafuta wapenzi kupitia mitandao ya kijamii.
Ujumbe uliomabatana na picha kwa mtandao huo wa kijamii ulielezea jinsi gani Nyota Ndogo aliyebatwiza jina la Sara, alivyobahatika kukutane na mpenzi wake aliyebatizwa jina la Raymond.
Msanii huyo alisema kuwa tayari kuna watu waliotapeliwa kupitia picha hio, akiadai pia nusra rafiki yake atoe hela kwa ajili ya kupata mpenzi wa mzungu.