Huku serikali ikijizatiti kuekeza kwenye mashirika inayomiliki, bado mashirika hayo yanakumbwa na matatizo si haba, ikiwemo kugoma kwa wafanyakazi pamoja na kupigwa kalamu kwa wafanyakazi wasiowajibika kazini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mashirika hayo hupata hasara kila mwisho wa mwaka huku baadhi ya vifaa vyao vikahariibika mara kwa mara.

Katika Kaunti ya Mombasa, Shirika a huduma za feri KFS pamoja na lile la Halmashauri ya Bandari KPA, yanaendelea kukumbwa na changamoto nyingi, huku wateja wakiachwa katika hali ya kutatanisha wasijue namna ya kupata huduma muhimu wanazohitaji.

KFS imekua na matatizo mengi ikiwemo feri kukwama mara kwa mara huku ajali zinazohusisha magari katika eneo hilo zikiendelea kushuhudiwa mara kwa mara, kisa cha hivi karibuni kikiwa basi aina la Smart kutoka nchi jirani ya Tanzania kutumbukia ndani ya Bahari hindi, baada ya kusemekana kupoteza mwelekeo.

Siku ya Alhamisi wiki iliyopita, kivuko cha Likoni kilishuhudia hali ya taharuki baada ya feri moja kukwama huku mamia ya abiria wasijue la kufanya.

Sio mara ya kwanza kwa feri kukwama katika eneo hilo, ila kinachoshangaza ni kwamba hakujachukuliwa hatua ya kukarabati na kuhakikishia feri hizo haziwezi kwama.

Halmashauri ya bandari nchini KPA, ni mojawapo ya shirika kubwa zaidi linaloleta kipato cha juu kwa taifa hili, ila wafanyakazi hugoma wakilalamikia mishahara, mazingira duni na hata kuhangaishwa na usimamizi wa idara mbalimbali wanazozifanyia kazi.

Wafanyabiashara wa kampuni zinazohudumu kwenye shirika hilo waligoma siko ya Alhamisi wakilalamikia mishahara yao, huku wengine wakikiri kutojulishwa sehemu ya kufanyakazi kama ilivyodesturi wanapofika kazini.

Huku hayo yakijiri, Shirika la ndege la Kenya Airways ambalo limekuwa likiyumbayumba kutokana na hasara waliyokadiria mwaka jana ya takribani bilioni 25, limepata hasara ya bilioni 26 mwezi huu.

Shirika hilo ambalo pia ni mojawapo ya mashirika tajika kote ulimwenguni limekuwa likikumbwa na msukomsuko wa kifedha uliopelekea wizara ya fedha kulifadhili zaidi ya mara mbili, huku msaada wa hivi karibuni ukiwa wa bilioni kumi.

Hiyo haikutosha kwani usimamizi wa shirika hilo uliamua kuwatimua wafanyakazi zaidi ya mia sita kama njia moja wapo ya kupunguza matumizi, ila hadi kufikia sasa bado shirika hilo halijaimarika vilivyo.

Swali ni , je, anayehusika kwa matatizo yanayokumba mashirika haya ni nani? Ni usimamizi ama wanaofanyabiashara kwenye mashirika hayo?