Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo. Picha/nation
Mbunge wa kisauni Ali Mbogo amewapa changamoto wabunge sita kutoka pwani ya Kenya kuwa watapoteza viti vyao vya kisiasa iwapo shida ya mashamba eneo hilo haitatatuliwa.
Wabunge hao wako katika kamati ya Kitaifa ya Mashamba katika bunge la kitaifa ya watu kumi na tisa
Viongozi hao wakiwemo Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati hiyo, Omar Mwinyi wa (Changamwe), Teddy Mwambire wa (Ganze), Mishi Mboko wa Likoni na Owen Baya wa Kilifi Kaskazini
‘‘Wakati huu iwapo shida ya Mashamba itaendelea kutuandama, inamaanisha wenzetu watakuwa wamezembea katika kazi yao. Lazima tutatue angalau asilimia 50% ya shida ya mashamba eneo hili la pwani,’’ Mbogo alisema.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa ni fursa ya kipekee ambayo watu wa pwani wamepewa ya kusuluhisha tatizo hilo.
Mbogo aliyasema haya mapema wiki hii wakati ambapo yeye na Mwashetani walikutana na maskwota wa mashamba kutoka eneo bunge la Kisauni .
Mkoa wa pwani una idadi kubwa ya maskwota wa Mashamba na Migogoro mingi ya Mashamba.
Kulingana na Mbogo,eneo bunge la Kisauni lina zaidi ya Maskwota elfu themanini. Khatib Mwashetani aliwataka wakaazi wa pwani kuwa na subira wakati swala la Mashambo linaposhughulikiwa.