Mkuu wa Idara ya Elimu katika serikali ya Kaunti ya Mombasa Tendai Lewa amesema kuwa atawania kiti cha useneta katika uchaguzi mkuu ujao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumanne, Tendai alisema kuwa amevutiwa na kiti hicho baada ya kuona ulegevu uliopo katika afisi ya seneta wa sasa.

Tendai ambaye aliwania kuwa gavana katika uchaguzi uliopita na kushindwa na Hassan Joho, alisema kuwa ameridhishwa na jinsi gavana huyo anavyoendesha shuguli ya kaunti hiyo na hivyo basi hatawania kiti hicho cha ugavana.

Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar alitangaza rasmi kuwa atawania kiti cha ugavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.