Mwakilishi wa Wadi ya Sengera Bosoti, Kaunti ya Kisii Timothy Nyarang’o, ameiomba Serikali ya Kaunti hiyo kutengea Wadi pesa kugegemea ukubwa au undogo wa Wadi hizo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na Mwandishi huyuwa Habari siku ya Jumatano, Nyarang’o alipendekeza kuwa Wadi kubwa zinastahili kutengewa pesa nyingi zaidi za maendeleo, kando na zile ndogo.

Nyarang’o amehoji kuwa Wadi kubwa na zile ndogo zikipokezwa pesa kiwango sawia, huenda zile kubwa zibaki nyuma kimaendeleo kwa kuwa si rahisi kuyatimiza mambo waliyowahidi wapiga kura kama hawapokezwi pesa nyingi kwani Wadi zao ni kubwa.

Mwakilishi huyo alisema kwamba Wadi yake ni miongoni mwa Wadi kubwa katika Kaunti ya Kisii na kumwomba Gavana wa Kaunti hiyo James Ongwae kujumuisha matakwa yao kwenye bajeti ya mwaka wa 2015/2016.

Aidha, Mwakilishi Nyarang’o amesema kuwa Wawakilishi wengine wa Wadi hawawezi kuzikarabati barabara zao kwa kilomita tatu, maana wakizitengeneza barabara hizo watavuka Wadi ya Wawakilishi wengine kwani Wadi hizo ni ndogo zaidi,” alisema Nyarang’o.

Wakati uo huo, Mwakilishi huyo amewaomba viongozi wote kuwafanyia wananchi maendeleo huku wakiyafuata yale waliyowaahidi wapiga kura wakati wa kampeini.

“Tutafurahi sana ikiwa Wadi zile kubwa zikitengewa pesa nyingi zaidi, kwani maendeleo yatatimizwa katika kila Wadi,” aliongezea Nyarang’o.