Aliyekuwa mbunge wa Lamu Magharib Julius Ndegwa akiwa mahakamani hapo awali. [Picha/ standardmedia.co.ke]
Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini amewasilisha ombi la kumuondolea aliyekuwa mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa mashtaka ya ufujaji wa fedha za CDF.Ombi hili limewasilishwa katika Mahakama ya Mombasa na naibu mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa Alexendra Muteti.Muteti amepokea agizo hilo kutoka kwa afisi kuu ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Keriako Tobiko, baada ya kuhisi ushahidi unaozidi kutolewa ni hafifu.Ndegwa alishtakiwa pamoja na maafisa wengine sita wa kamati ya hazina ya CDF ya eneo bunge la Lamu Magharibi.Wasaba hao wanadaiwa kushirikiana kuiba shilingi milioni mbili kutoka hazina hiyo ya CDF.Tayari zaidi ya mashahidi kumi wametoa ushahidi wao kuhusiana na kesi hiyo.Hakimu Julius Nange’a atatoa uamuzi kuhusu kesi hiyo tarehe Oktoba 19, mwaka huu.