Viongozi wa muungano wa Cord wameshauriwa  kuandikisha taarifa dhidi ya madai kuwa wanajua aliyetekeleza mauaji ya mwanabiashara mashuhuri jijini Nairobi Jacob Juma aliyezikwa Jumamosi wiki jana huko Bungoma.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ni wito uliotolewa na viongozi wa makanisa mbalimbali katika eneo la Rongai siku ya Jumatatu.

Wakizungumza na mwandishi huyu adhuhuri ya Jumatatu katika eneo la Mogoiwet, viongozi hao walisema kuwa taarifa hizo zitasaidia maafisa wa polisi kwenye uchunguzi dhidi ya mauaji hayo.

Kiongozi wa kanisa la Gospel Evangelism Mark Waweru alisema; “Viongozi wa muungano wa Cord wamekuwa wakitilia siasa kwenye swala hili jambo ambalo halifai hata kidogo.”

Francis Kurui wa kanisa la Redeemed Gospel Ministry naye alisema; “Maafisa wa polisi wanapaswa kupewa muda wa kutosha kufanya uchunguzi wao, ili wahusika wapate kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.”