Mzozo ya kisiasa umetokea katika kundi la Maseneta kutoka kanda ya Pwani siku chache tu baada ya kundi hilo kubuniwa na viongozi hao huku baadhi yao wakidai kuwa hawakuhusishwa katika muundo wa kundi hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hata hivyo Katibu wa kundi hilo ambaye pia ni Seneta wa Mombasa Hassan Omar amepuzilia mbali madai hayo na kusema kuwa Maseneta wote wa Pwani walikuwa wamehisishwa na kushauriwa vilivyo huku akisema kuwa kundi hilo litazunduliwa rasmi mwezi wa Mei.

Aidha Bw Omar ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano na wakaazi wa Likoni siku ya Jumamosi amesema kuwa kulikuwa na haja ya kubuni kundi hilo kwa kuwa Maseneta kutoka kanda ya Pwani walikuwa hawatambuliwi na lile kundi la Wabunge kutoka kanda ya Pwani.

Haya yakijiri, Seneta Mteule Emma Mbura amesema kuwa uchaguzi wa viongozi wa kundi hilo haikutilia maanani nafasi ya viongozi wanawake na hivyo kutaka uchaguzi wa viongozi urudiwe tena.