Katika njia mojawapo ya kuwapa nguvu kina mama kiuchumi, mbunge wa Nyaribari Chache Richard Tong'i amejitolea kuyasaidia makundi ya kinamama kwa kuwakopa hela za kuwakimu kiuchumi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge huyo, akiongea siku ya Jumanne katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali kwenye eneo bunge lake, Tong’I aliwataka kina mama kuendelea kujiunga. kwa makundi ili wapate mikopo ambayo amewatengea kwenye pesa za maendeleo ya maeneo bunge CDF, ambapo alidokeza kuwa ameweka hela kando mahusus kwa vijana na kina mama.

Tong'i aidha aliwataka wote wanaotuma maombi ya pesa za mikopo kuzitumia vizuri wanapofaulu kupewa na kamati za CDF, au taasisi nyingine za kifedha ili kutoa nafasi nzuri wengine kupata.

“Tumieni hela za mikopo vizuri ndio inakuwa rahisi kupewa tena na wengine kuwa rahisi kuzipata kupitia faida inayotokana na pesa hizo; jiunge pamoja kwa makundi, maana hiyo ni njia moja ya kupata pesa hizo rahisi kuliko kuwa mmoja,” alihoji Tong'i.

Mbunge huyo aliweza baadaye kutoa pesa za msaada wa karo kwa wanafunzi wasio na uwezo kifedha katika eneo bunge lake.