Huenda hali ya vuta nikuvute ambazo zimekuwa zikishuhudiwa baina ya chama cha walimu nchini Knut na tume ya kuajiri walimu nchini TSC, zikazikwa katika kaburi la sahau baada ya pande hizo mbili kutia sahihi mkataba wa makubaliano utakaowawezesha kufanya kazi kwa pamoja.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumanne, katiku mkuu wa chama cha Knut Willson Sossion, alisema kuwa mkataba huo unanuia kuhakikisha kuwa makubaliano ya hapo awali kuhusu nyongeza ya mishahara pamoja na marupurupu za walimu yametekelezwa kulingana na katiba.

Aidha, mwenyekiti wa tume ya kuajiri walimu nchini TSC Lydia Nzomo alisema kuwa stakabadhi hizo muhimu zitahakikisha kuwa uhusiano mwema unarejea katika sekta ya elimu.

“Mkataba huo utahakikisha kuwa migomo ya walimu wakilalamikia nyongeza ya mishahara haishuhudiwi tena,” alisema Nzomo.