[Photo/courtesy]Huenda idadi ya siku za kufanyika kwa kongamano la walimu wakuu wa shule za upili linalofanyika kila mwaka kaunti ya Mombasa ikapungua hadi siku mbili kutokana na idadi kubwa ya walimu kukosa kuhudhuria kongamano hilo.Haya yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa TSC Nancy Macharia wakati wa kufunga rasmi kwa kongamano hilo lilodumu kwa siku 5 , amedai asilimia kubwa ya walimu huja Mombasa na kutumia fursa hiyo kujivinjari badala ya kuhudhuria kongamano hilo.Macharia aidha ametoa wito kwa walimu wakuu na walimu wote kwa jumla kuhakikisha wanajukumika bila ya kushurutishwa ili kuhakikisha wanapeleka gurudumu la elimu nchini mbele.
MOMBASA
TSC yatishia kupunguza siku za kongamano la walimu wakuu mwakani
ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Wesley Wesonga