Familia katika Kaunti ya Kisii zimeombwa kujitokeza na kupigana na funza ambazo zimevamia watu wengi katika eneo hilo.
Kepha Keng'oina mhudumu wa afya katika eneo la Kisii amesema kuwa watu wengi katika maeneo hayo wameadhiliwa na funza kwa kukosa kuzingatia usafi.
“Lazima sisi kama wakaazi tuwajibike na kutunza mazingira ili kuepuka maradhi,” akasema Keng'oina.
Keng'oina alikuwa akiongea wakati alipozuru familia moja ambayo imeadhiliwa na funza katika eneo la Nyanchwa kaunti ya Kisii.
“Familia hizi zinahitaji funzo maalumu jinsi ya kujikinga na kuepukana na funza hao,” alisema King’oina.
Aidha Keng'oina ameiomba serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati na kushilikiana na sekta ya afya kupigana na funza.