Wanabiashara kutoka soko la Gesima Kaunti ya Nyamira wamelalama kwa serikali ya kaunti hiyo kutokana na kukosekana kwa vibanda vya kujikinga na mvua wakati wanafanya biashara zao.
Wakiongea katika soko hilo siku ya Jumapili katika soko hilo, wanabiashara hao walilalama kutokana na kunyeshewa hasa wakati wa msimu wa mvua katika jimbo hilo, na kuwasababishia hasara kubwa kwa kuwa hakuna mahali pa kujingika na hata kuweka bidhaa zao.
Mama salome Kenyoni, ambaye ni mwanabiashara mmoja wa soko hilo ameeleza kuwa huchukua bidhaa zake katika soko hilo, lakini wakati mvua inaponyesha hupata hasara kubwa kwa kuwa hauzi kitu chochote na hata bidhaa wanazouza uwa na matope, jambo linalochangia wanunuzi kutonunua.
“Wakati mvua inaponyesha, mimi hupata hasara nyingi kwa kuwa hatuna mahali pa kujikinga wakati mvua inanyesha na uharibu bidhaa zangu, kitu ambacho uniuwa moyo kwa kuwa nategemea biashara hii,” alisema Kenyoni.
Aidha, wanabiashara hao wamemkashfu mzee mmoja ambaye hutumia uwanja huo kuwalisha punda zake, ambao huchafua uwanja huo na wanabiashara hao wameomba manisipaa ya Nyamira kumchukulia hatua mzee huyo kwa kuwa wanaofya afya yao .
Kwingineko wamemwomba mwakilisli wa wadi hiyo ya Gesima Kennedy Nyameino kushirikiana na serikali ili kujenga vibanda hivyo na wajiendeleze na biashara zao kwa kuwa wengi hutegemea biashara hizo.
Kwa upande mwingine, wameiomba manisipaa ya Nyamira kujenga Vyoo vya usafi, kwa kuwa kwa sasa wanatumia vyoo vya kituo cha kununulia majani chai kilicho karibu na soko hilo, kitu wemesema ni kinyume na matarajio yao kwa kuwa wanatozwa ushuru kila siku ya soko na wanatarajia pesa hizo kutumika kwa ujenzi huo.