Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Aliyekua kwa wakati mmoja Waziri wa Maswala ya Nje Raphael Tuju amepuuzilia mbali madai yanayoenea kuwa anazuiliwa nchini Tanzania, baada ya kutiwa mbaroni kwa madai ya kuhusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo jirani.

Akiwahutubia wanahabari, waziri huyo wa zamani alikanusha madai hayo ambayo yamekua yakienea mtandaoni, na kusema kuwa endaopo yangekuwa ni ya kweli, basi kila mtu angefahamu jambo hilo.

“Kumekuwepo na habari kuwa nilitiwa mbaroni na kuzuiliwa nchini Tanzania. Endapo ni kweli nilikuwa nimefungwa, nyinyi hamuoni swala kama hili lingekuwa limemfikia kila mtu na kuwa jambo kubwa hasaa mkizingatia cheo changu cha awali cha aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni?” aliuliza Tuju.

Kuhusiana na swala la siasa za humu nchini, Tuju alisema kwa sasa hana nia ya kuwania nafasi yoyote ya kisiasa kama inavyodaiwa.

“Nawahakikishia kuwa sina mpango wowote wa kuwania wadhifa wa urais katika uchaguzi mkuu ujao,” alisema Tuju.