Wakaazi wa eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira wamemwomba mbunge wa eneo hilo Timoty Bosire kuzikarabati baadhi ya bababara.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea siku ya Ijumaa katika sehemu ya Rigoma wakati wakipokea pesa zao za chai, wakazi hao walisema kuwa barabara za eneo bunge la Kitutu Masaba tangu Kenya ijinyakulie Uhuru ziko kwa njia mbovu, na hasa wakati huu wa mvua hazipitiki.

Kwa sasa, wakazi hao wamemuomba mbunge wao kuzikarabati, ili uchukuzi unawiri katika sehemu hiyo.

“Tunamuomba mbunge wetu kuzikarabati barabara hasa zile zinasimamiwa na serikali kuu kwa kuwa yeye hutuwakilishi katika serikali Kuu,” alisema Monda Joseph, mkazi.

Baadhi ya barabara mbovu katika eneo hilo ni ya kutoka Manga kuelekea Esaba, ambayo kwa sasa haipitiki, ambapo huwabidi watu kutembea na miguu hadi kwa ofisi za kaunti ambazo ziko Sehemu ya Manga kwa kuwa hamna gari wala pikipiki inayopita hapo kwa kuwa barabara hiyo ina matope mengi.

Kwingineko, wanaotumia barabara ya Metamaywa kuelekea Kebirigo wameiomba serikali kuu kumaliza barabara hiyo, ili waweze kuitumia hasa wakati huu wa mvua nyingi.

Kulingana na wakazi hao, barabara hiyo, ambayo inaendelea kukarabatiwa na kampuni moja kwa sasa iko katika hali mbaya kushinda hapo awali, kama sehemu ya Nyabiosi  na Monchewa, kutokana na kulimwa na trakta.

Kwa sasa wameiomba serikali kuu kuharakisha kukarabati barabara hiyo ili kurahisisha uchukuzi.

“Tunaiomba serikali kuu kuharakisha ujenzi wa barabara hii kwa kuwa wakati huu wa mvua barabara hii imekuwa mbaya zaidi hata kushida hapo awali,” alihoji mzee Daniel Kegoro.

Aidha, wamesema wamekuwa gizani kwa takribani majuma matatu kwa kwa kuwa stima ilitolewa ili isongezwe kutoka barabarani na hadi sasa bado kuunganishwa.