Wakaazi wa Lokesheni ya Mwamonari, Wadi ya Sensi kutoka eneo Bunge la Kitutu Chache Kaskazini katika Kaunti ya Kisii wameiomba Serikali ya Kaunti hiyo kuwatengenezea chemichemi ya maji ya Isambo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakionyesha ghadhabu yao siku ya Jumanne, baadhi ya wakaazi kutoka enero hilo Lydiah Kerubo, Ruth Bakari na Elizabeth Moraa ambao ni miongoni mwa wachota maji katika chemichemi hiyo ya maji walisema kuwa wamekuwa wakisumbuka hasa watu wanapokuwa wengi kwa kupanga foleni ndefu ili kuchota maji hayo.

“Tunaomba Serikali ikarabati mto huu na tuwekewe chuma zaidi ya tatu za kuvuja maji ili tusiwe tunaongojea kwa muda mrefu kwa kuchota maji,” alihoji Kerubo.

Wakati uo huo, wakaazi hao waliosema itakuwa furaha kwao watakapokarabatiwa chemichemi ingine mbadala kwani ni wengi wanatumia chemichemi hiyo ya maji ilioko eneo la isambo, ambayo inawabidi kuchelewa kufika nyumbani mapema na kulaumiwa na mume zao.

“Tukiwa wengi hapa tunapanga foleni na tunachelewa kufika nyumbani mapema, jambo ambalo linatusababishia kugombanishwa na mume zetu. Tunaomba kama hatutatengenezewa chemichemi ingine, watuwekee chuma zaidi ya tatu ambazo zitatuwezesha kuchota maji kwa haraka,” aliongezea Kerubo.

Wachota maji hao walisema kuwa hawajafurahia matunda ya ugatuzi kwa sekta ya maji hata hivyio, wamekubali kuwa Serikali ya Kaunti hiyo imejaribu katika sekta zingine mbali mbali.