Naibu Gavana wa kaunti ya Mombasa Hazel Katana amepuzilia mbali maadai kuwa kuna uhasama baina yake na gavana wa kaunti hiyo Hassan Joho.
Akiongea kwenye mkutano na akina mama siku ya Alhamisi, Katana ameapa kuwa ataendelea kufanya kazi na gavana Joho na kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao.
Katana pia amewashauri kina mama kujitokeza ili kuwania nafasi za uongozi ili kuboresha kaunti ya Mombasa, akisema kuwa kina mama ndio marafiki wakuu wa maendeleo.
Hapo awali kulikuwa kumetokea tetesi kuwa Katana na Joho walikuwa hawaonani macho kwa macho baada ya naibu gavana huyo kupinga uamuzi za Joho Kuhusu vile serikali ya kaunti hiyo inavyoendeshwa.