Baada ya maandamano ya wanacord kuzimwa katika kaunti ya Nyamira siku ya Jumatatu, vijana hao wameapa kuendelea na maandamano hayo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na mwenyekiti wa vijana wa ODM kaunti ya Nyamira Dennis Marube, maandmano ya Jumatatu ilikuwa jaribio, lakini Jumatatu ijayo ndio maandamano yenyewe ambayo aliyaita maandano 'baba yao'.

"Tunaandaa na kupanga maandamano baba yao wiki ijayo, kwa kuwa ya wiki hii ilikuwa tu matayarisho na jaribio la maandamano," alisema Marube.

Maandamano ya wanacord Nyamira yalizimwa baada ya mkuu wa askari wa kituo cha Nyamira kuwaamurisha wazidishe maandamo hayo kwa kuwa hawakuwa na kibali cha kuandamana . 

"Nawaomba mzidishe maandamano haya kwa kuwa hamna kibari cha kuandamana," aiwaomba afisa huyo.

Sasa bwana Marube na kundi lake wameapa kutolegeza kamba ya maandamo hadi afisi ya tume ya IEBC na makamishena hao wangatuke afisini.