Vijana wa shirika la Huduma kwa Taifa (NYS) katika eneo bunge la Nyaribari Chache wameshauriwa kutumia vyema pesa wanazopata kutoka katika mradi huo ili kujiendeleza katika jamii.
Ushauri huo umetolewa baada ya kubainika kuwa wengi wao hawatumii pesa hizo vyema ili kujisaidia katika siku zijazo.
Mwenyeki wa vijana hao wa katika eneo bunge hilo la Nyaribari Chache Edward Nyatari alisema vijana 1,000 walifanikiwa kupata fursa ya kufanya kazi hiyo na kusema ni muhimu kwao kutumia vyema pesa hizo kwa kuwekeza ili kujiendeleza.
“Vijana hawa hupokea pesa baada ya kila juma moja nawaomba wote kuzitumia vyema ili kujiendeleza kimaisha,” alisema Nyatari.
“Kazi hii ya huduma kwa vijana imeng’oa nanga rasmi hii naomba kila kijana kuwa na fikira za kujifaidi kutoka huduma hii,” aliongeza Nyatari.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alipongeza serikali kwa kuleta huduma hiyo katika eneo bunge hilo.