Aliyekuwa Diwani wa wadi ya Kerema Riuri inayojulikana kama Masimba ward kwa sasa, katika eneo bunge la Nyaribari Masaba kusini, kaunti ya Kisii Kennedy Okindo Nyabuga emetoa wito kwa serikali kuu kuwafidia pesa walizofanyia kazi ya serikali wakati wa Rais Mwai Kibaki. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza nasi mjini Kisii, Okindo, aliyekuwa mwenyekiti wa madiwani katika eneo bunge la Nyaribari Masaba Kusini, amemwomba mbunge wa eneo hili Elijah Moindi kuwasilisha mswada huo bungeni. 

Pia ametoa shukrani kwa serikali ya Rais Kenyatta kwa kujali maisha ya wakongwe. 

“Eneo bunge hili la Nyaribari Masaba Kusini tuko na madiwani mia tatu ambao tulifanya kazi katika serikali miaka mingi," alisema Okindo.

"Tunashukuru serikali ya mheshimiwa Uhuru kwa kujali maisha ya wazee wakongwe ili nao wapate fidia ya uzeeni. Na sisi kama wale madiwani wakongwe ambao tulifanya kazi wakati wa Kibaki tunaomba serikali ituangalie," aliongeza Okindo.

"Pia ninamuomba mbunge wetu Elijah Moindi awasilishe mswada huu bungeni ili nasisi tuangaliwe kwasababau sisi ndio tulitengeneza njia nzuri pia tuna watoto nyumbani ambao wanatutegemea," alikariri Okindo.

"Wengine wanateseka kwasababu ya umaskini na hata wamekufa bila kuziona pesa hizo. Kwa hivyo ni ombi langu kuwa serikali itasikia na kutujali. Mswada huu ulipitiswa na maseneta, pia wabunge wetu wauangalie watusaidie,” alisema Okindo.