Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Eramba iliyoko wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini Kaunti ya Kisii Samuel Mweruti, ameiomba serikali ya kaunti ya kuisaidia kwa ujenzi unaondelea katika shule hiyo.
Alikuwa akiongea katika shule yake ya Eramba wakati wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa kidato cha nne mwaka jana walikuwa wakikabidhiwa zawadi mwalimu huyo aliomba serikali kuisadia kwa ujenzi wa madarasa.
Tuko na upungufu wa madarasa katika shule yetu na mwaka huu wanafunzi wameongezeka maana wanafunzi katika kidato cha kwanza wako 103 na tunahitaji madarasa mengi zaidi,”alisema Mweruti mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“Tayari tumeanzisha ujenzi wa madarasa mengine na tunaomba serikali ya kaunti yetu itusaidie kwa unjenzi huo ili ukamilike haraka,” aliongezea Mweruti.
Aidha mwalimu huyo alikiri kuwa ujenzi ambao umeanza ulianzishwa kufuatia na kujitolea kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na zile pesa walikabidhiwa kutoka hazina ya ustawi maeneo bunge CDF ambazo alikiri kuwa hazitoshi.
Shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwa miaka mingi iliopita jambo ambalo liliwapelekea wazazi kuwachua watoto wao wengi katika shule hiyo na kusababisha upunguvu wa madarasa.
Sasa kibarua ni kwa serikali ya kaunti ya kisii ikiongozwa na gavana James Ongwae kusaidia shule hiyo kwa ujensi huo kama njia mojwapo ya kuinua viwango vya masoma juu katika shule za eneo la Kisii.