Nasuri almaarufu Fistula ni hali ambayo imewasumbua na kuwapa aibu wanawake wengi nchini Kenya na hata katika kaunti ya kisii.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanawake waja wazito huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na hali hii ya aibu ambayo hutokana na shimo lisilo la kawaida linalo pasuka kati ya uke na kibofu kwa mwanamke. Hali hii hutokea wakati mwanamke mja mzito anapohisi uchungu wa uzazi kwa muda mrefu.

Akizungumza nasi katika hospitali ya Gynocare, Kisii, mkurugenzi wa shirika la Wakfu wa Fistula Daraja Mbili, Elkanah Ntabo amedokeza maana ya jina Nasuri na njia za kutibu shida hii.

“Mwanamke aliye na Nasuri hupoteza uwezo wake wa kuzuilia mkojo au choo hali ambayo humpekelea kutiririkwa na mkojo au choo kumtoka bila kizuizi, wakati wowote usiku na mchana," alieleza Ntabo.

"Hii ni hali ya wakati mwanamke anaposhika mimba kwa kawaida huwa ni wakati wa furaha. Hata hivyo hali hii humtatanisha na humpelekea kujitenga kutoka kwa jamii au hata kutengwa na jamii na familia na kuishi maisha ya upweke,” aliongeza Ntabo.

Pia daktari alizidi kueleza njia ambazo mwanamke atatumia ili kupata matibabu ya bure.

“Nasuri inaweza kutibiwa kwa kufanyiwa upasuaji. Hata hivyo, madaktari walio na ujuzi wa kufanya upasuaji huu ni wachache na gharama yake ni ya juu sana," alieleza Ntabo.

"Ni kwasababu hii ambayo shiririka la Freedom From Fistula Foundation lilianzishwa ili kuangazia hali hii na kutoa tumaini kwa waadhiriwa bila malipo yoyote," alisema daktari.

"Mwanamke aliye na hali hii anapewa matibabu ya bure hata kama mwadhiriwa anatoka mbali atasafirishwa na gari bila kulipa chochote,” aliongeza Ntabo.