Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae amekiri kuwa wabunge hawatakufa moyo kupitisha mswada wa kijinsia uliokosa kupita siku ya Alhamisi bungeni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na Chae wabunge wataendelea na kampeini ya kuhakikisha mswada huo umepita bungeni baada ya miezi sita ili kuwapa fursa wanawake kutosahulika katika teuzi za bungeni.

“Wengi walidhani kuwa mswada ungepita wanawake wangenyakua uongozi na kupendelewa, mswada huu ungesaidia wanawake kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali bungeni na serikali ili uongozi kuwa sawia kati ya wanaume na wanawake,” alisema Chae.

Chae aliasa wabunge kuwa wakati mswada huo utarejeshwa bungeni waweze kuupitisha kuonyesha usawa na uwazi kwa uongozi katika taifa la Kenya.

“Naomba wakati ujao tutakaporejelea bungeni tuupitishe mswada huo wa kijinsia kulingana na katiba maana sisi sote sharti tujali maslahi ya kila mmoja nchini,” aliongeze Chae.

Mswada huo ulitupiliwa mbali na Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi siku ya Alhamisi baada ya kukosa idadi iliyohitajika ya wabunge ile kuupitisha.