Wafanyibiashara katika soko la Ikonge, kaunti Nyamira wameiomba manispaa ya kaunti ya Nyamira kushirikiana na sekta ya afya kutoa uchafu katika soko hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea siku ya Ijumaa katika soko hilo lililoko katika kaunti ya Nyamira, baadhi ya wanabiashara walilaaumu manispaa ya kaunti hiyo kwa kutatoa uchafu katika soko hilo, huku wakiwaomba wasimamizi kushughulikia jambo hilo kwa haraka, kwa kuwa magonjwa yanaweza kurupuka kutokana na uchafu huo.

Wanabiashara hao ambao walionyesha kutofurahishwa na wasimamizi wa soko hilo walisema kuwa wasimamizi hao hawawajibiki na kazi yao kwa kuwa kama wangekuwa wanawajibika, uchafu huo ungekuwa umetolewa mahali hapo na kuchukuliwa mahali kunapostahili.

“Ni aibu kubwa kuwa na uchafu mwingi katika soko letu na kuna vyakula na mboga ambazo wengine wetu tunaunza na hakuna mwenye ananunua kwa kuwa soko letu ni chafu,” alihoji Gesare.

Aidha, wameiomba serikali ya kaunti Nyamira kuingilia kati na kuwasaidia kwa kuwa wengi wao wamehofya afya yao kwani huenda uchafu huo ukasababisha magonjwa haswa ugonjwa wa Kipindupindu.

“Tunaomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuingilia kati na kuleta suluhu mwafaka ili kukinga kutokana na magonjwa ambayo yataweza tokea kutoa kwa uchafu huu,” alihoji Fred Mochama, mwanabiashara wa Nguo.

Kwingineko, wanabiashara hao wamewaomba wenzao wanaopika vyakula katika soko hilo kuzingatia usafi huku wakiongojea hatua ya serikali ya kaunti ya Nyamira itachukua kushugulikia swala hilo la usafi.