Viongozi na jamii katika eneo la Gusii wameombwa kusaidia kutambua wakimbizi wa ndani kwa ndani halisi ambao wanafaa kufidiwa na serikali ya kitaifa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya kubainika kuwa kuna wakimbizi bandia ambao wanahitaji kufidiwa hukuuhalisi wao ukiwa ni wakupigiwa shaka.

Akizungumza Jumatatu usiku kwenye mahojiano katika redio ya Egesa Fm, Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali ya kitaifa inapania kuwafidia wakimbizi katika eneo la Kisii huku akiomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na jamii ili kutambua wakimbizi halisi ili wapate kufidiwa.

Kenyatta alisema baadhi ya watu wanajifanya kuwa wakimbizi ili kufidiwa jambo ambalo alisema halina msingi wowote.

“Wakimbizi wajanja hawatafaidika kutoka kwa serikali na ninaomba jamii na viongozi wa Kisii tushirikiane kujua wakimbizi halisi ili wafidiwe,” alisema Kenyatta.

Kenyatta aliwahakikishia wakimbizi wa eneo la Kisii kuwa watafidiwa baada ya wakimbizi halisi kutambuliwa huku akisema ni ratiba inafutwa wala sio kulipwa mara moja.