Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho ametoa wito kwa seneta wa kaunti hiyo Hassan Omar na viongozi wengine katika kaunti hiyo, kuungana pamoja katika kuhakikisha kuwa Mombasa inaendelea.
Akizungumza katika hafla ya kuzindua Ruwaza wa 2035 siku ya Jumamosi, Joho alisema kuwa ushauri wa viongozi wote wa kaunti hiyo unahitajika ili kuhakikisha kuwa maarifa zaidi yanapatikana ya kuendeleza kaunti hiyo.
“Sina uhasama na kiongozi yeyote na niko tayari kushirikiana na viongozi wote katika kuboresha maisha ya wakaazi wa Mombasa,”alisema Joho.
Haya yanajiri baada ya Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar kudai kuwa serikali ya Kaunti ya Mombasa haijakuwa ikimhusisha katika kufanya uamuzi muhimu unaochangia maendeleo ya kaunti hiyo.