Seneta wa Kaunti ya Kisii Chris Obure amewaomba Wakaazi wa Kaunti ya Kisii kushirikiana na viongozi wote ili kuinua viwango vya maendeleo katika Kaunti hiyo.
Vile vile, wanao azma ya kuwania viti mbalimbali katika Kaunti Ya Kisii wameombwa kushirikiana na kuwaunga mkono viongozi walioko ofisini kwa sasa ili kuimarisha viwango vya maendeleo katika Kaunti hiyo.
Akiongea katika hafla ya wanachama wa muungano wa wanachama wa CORD siku ya Jumapili, Seneta Obure, amewaomba watu wote kushirikiana kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika eneo hilo.
“Kwa kuleta maendeleo ni lazima tushirikiane kwa pamoja na kuhakikisha kuwa mwanaichi wa kawaida anafaidika,” alisema Obure.
Kwingineko amewaomba wanao azma ya kuwania kiti chochote katika Kaunti ya Kisii kuweka azma yao kando na kushirikiana na viongozi waliomamulakani kwa sasa.
“Ili maendeleo yaendelee katika Kaunti yetu lazima sisi viongozi na wapinzani tushirikiane na kuacha kuonyeshana vidole vya lawama kila wakati,” alisema Obure.
Kwa upande wake Mbunge wa Nyaribari Masaba Elijaah Moindi naye amewaomba watu wote kushirikiana huku akiwaonya wanakandarasi wote waliopewa kazi ya kujenga barabara katika eneo Bunge lake kufanya kazi ipasavyo.
Akiongezea amewaomba wanakandarasi hao kuwajibika kwa kazi yao ili kuepuka mizozo ya kila wakati nakutengenezwa kwa kila mara.
Vile vile Mbunge huyo amepongeza kuwa wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa mwaka jana. Moindi amesema ataendelea kuunga mkono masomo katika eneo Bunge lake na kuhakikisha kuwa wanafunzi watafanya vyema zaidi mwaka huu.