Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir katika hafla ya awali.[Picha Abdulswamad Nassir/ Facebook]
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir amesema atakuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kinara wa NASA Raila Odinga anapishwa kuwa rais.Akizumgumza siku ya Jumapili katika Kaunti ya Kilifi, Nassir alisema kuwa atashirikiana na viongozi wengine wa NASA kuhakikisha kuwa Raila anaingia ikulu ya rais.“Tutashirikiana kwa hali na mali hadi Raila atakapoingia ikulu. Tutamuapisha bila kujali,” alisema Nassir.Nassir alisema kuwa Raila amepigania haki za Wakenya kwa muda mrefu sana na kuongeza kuwa kinara huyo wa mrengo wa upinzani anastahili kuwa rais wa Kenya.“Raila amepigania haki za wanyonge kwa muda mrefu huku akidhulumiwa bila kuvunjika moyo. Sasa ni zamu yake aweze kuingia ikulu,” alisema Nassir.Mbunge huyo alisema kuwa eneo la Pwani limekuwa likimuunga mkono Raila kwa miaka mingi na wakati umefika wa kiongozi huyo kuapishwa ili aweze kuwahudumia Wakenya.Aidha, Nassir alisema kuwa uongozi wa Kenya unapaswa kuzunguka katika jamii zote za Kenya bali sio kunufaisha makabila mawili peke yake.“Uongozi wa Kenya sio wa makabila mawili pekee, lazima uongozi uzunguke katika makabila yote nchini mpaka yale yaliyotengwa,” alisema Nassir.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6