Gavana wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet Alexs Tolgos amesema kuwa watashirikiana na Chuo Kikuu cha Kisii kuendeleza masoma katika kaunti hiyo.
Akiongea siku ya Jumanne katika chuo cha Kisii katika hafla ya kukabidhiwa tawi la chuo cha Kisii, Tolgos alisema atashirikiana na chuo cha Kisii ili kuinua viwango vya masomo katika kaunti ya Elgeyo marakwet..
Haya ni kutokana na chuo cha Kisii wakishirikiana na serikali ya kaunti hiyo kufungua tawi la chuo cha Kisii katika kaunti ya Elgeyo marakwet ambacho ni Chebara .
Tawi hilo lilikabidhiwa kwa serikali ya Elgeyo Marakwet naye naibu msimamizi mkuu John Akama, ambaye allisema watashirikiana na serikali ya Kaunti hiyo ili kuendelea kuinua sekta ya elimu nchini.
Aidha, gavana huyo alisema kuwa yeye na serikali ya kaunti yake watahakikisha kuwa tawi hilo litaendelea kunawili katika sehemu hiyo.
“Serikali yangu na washikadhau wote tutahakikisha kuwa sekta ya elimu imeinuka kutokana na tawi hili la chuo cha Kisii na tutaweza kutoa msaada wetu kwa tawi hilo,” alisema Gavana.
Kwingineko, alipongeza washikadhau wote wa chuo cha Kisii kwa kuifanya kile vyuo vingine havijafanya, na kufungua tawi lao katika kaunti hiyo kwa kuwa wanafunzi kutoka sehemu hiyo watapata mahali pa kujiunga na kuendelea na masomo yao.
Kwa upande wake, Akama amewaomba watu wote kutoka kaunti ya Elgeyo Markwet kuunga mkono sekta ya elimu ili viwango vya masomo vinawili kila kuchaao.