Mwakilishi wa wanawake Mombasa Mishi Mboko amesema kuwa viongozi wote watakaowania nyadhfa zozote Pwani kupitia JAP watashindwa na wale wa Cord.
Mishi mboko ambaye pia amejitokeza kukashifu serikali kwa kumpokonya gavana wa Mombasa Hassan Joho walinzi na pia kumuagiza kurudisha silaha zote amesema kuwa mbinu hizo za serikali ni za kidikteta na wala hazifai kutumiwa wakati kama huu.
"Serikali ya JAP imeonyesha wazi kuwa wakishindwa kidemikrasia wanatumia udiktetea na nguvu za mabavu,” alisema Mboko.
Aliwatahadharisha viongozi wa Pwani kuwa makini sana na njama ya serikali.
Wakati huo huo Mishi Mboko pia amewataka viongozi wa Cord wanaoshirikiana na serikali kusiritisha uhusiano wao mara moja na kurejea katijka mrengo wa Cord akisema kuwa baada ya uchaguzi mkuu ujao ni wao wataunda serikali na kukomboa wakaazi wa Pwani.