Wafanyibiashara wote wa kaunti ya Kisii wameombwa kuunga mkono mradi mpya wa ukusanyaji ushuru katika kaunti hiyo ili kufaulu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mradi huo mpya wa kukusanya ushuru kupita njia ya kidigitali umesemekana kuwa huenda ukapunguza wezi wa ushuru ambao hutolewa katika kaunti hiyo.

Kulingana na gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae aliyezungumza mjini humo aliomba wafanyibiashara wote wa kaunti hiyo kuunga mradi huo wa kukusanya ushuru kwa njia hiyo ya kidigitali.

“Baada ya serikali yangu kutia sahihi ya maelewano na benki ya KCB na chuo kikuu cha Strathmore sasa ushuru utakuwa ukitozwa kidigitali ili tuokoe pesa nyingi ambazo zinadaiwa kuingia mifuko mwa watu binafsi,” alisema Ongwae .

“Naomba kila mmoja awe mfanyibiashara au la auunge mkono mradi huo mpya ili tusonge mbele pamoja,” aliongeza Ongwae .

Ongwae alisema atajaribu kila awezalo kuona kuwa kaunti hiyo imeinuka kibiashara na kufanya maendeleo mengi kulingana na ahadi alizowapa wananchi.

“Nimetengeneza soko za kaunti yangu na ninaendelea kutengeneza maana tunahitaji maendeleo zaidi,” alisema Ongwae.