Serikali ya kitaifa imehimizwa kuanzisha mradi kwa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) katika kaunti ya Nyamira kama ilivyo kwemgineko.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa baada ya mradi huo kutoanzishwa katika kaunti hiyo huku serikali ikiombwa kujali maslahi ya vijana wa eneo hilo.

Wakizungumza siku ya Jumanne mjini Nyamira vijana wa kaunti hiyo wakiongozwa na msimamizi wao Duke Masira walisema hawana kazi ya kufanya na kuomba serikali ya kitaifa kuanzisha mradi huo ili kuwanufaisha kimapato.

“Katika kaunti jirani ya Kisii kuna mradi wa NYS lakini hapa kwetu hakuna mradi huo haupo tunaomba serikali kuu kutukumbuka kama vijana na kuleta mradi huo huku pia,” alisema Masira.

Wakati huo huo , vijana hao waliwalaumu viongozi wa kaunti hiyo kwa kutowapigania kwa serikali ili kusaidiwa huku wakisema wakati Rais alifanya ziara yake katika kaunti hiyo viongoizi hao hawakumwambia rmahitaji yao.