Mbunge wa Jomvu Twalib Badi amewatahadharisha viongozi katika eneo bunge lake dhidi ya kuanza kampeni za mapema na kusitisha miradi za maendeleo katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya vijana wanaomuunga mpinzani wake mkono katika kinyanganyiro cha ubunge Philip Nzai kufumania mkutano wa harambee aliyokuwa akiongoza Bw Badi siku ya jumamosi huku wakiimba nyimbo za kumsifu Nzai.

Juhudi za wazee katika eneo hilo kuwatuliza vijana hao ziligonga mwamba huku mbunge huyo akilazimika kukatiza hotuba yake na kuondoka.