Ubaguzi wa kazi ndio unaochangia ukosefu wa kazi nchini na Afrika kwa jumla, hii ni kulingana na Profesa Jesse Roll wa chuo kikuu cha Baraton.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza mjini Eldoret alipoongoza sherehe za kufuzu kwa mahafala 60 wa taasisi ya kibinafsi ya mafunzo ya kiufundi na teknolojia, Roll alisema kwamba vijana wengi huchagua kazi ambazo wao hufanya, huku wengi wakingoja kuajiriwa.

kulingana na Roll, hali hii huchangia kutoendelea kwa mataifa ya Kiafrika.

Baadhi ya mahafala hao wanatoka Kaunti ya Turkana, na walikuwa wakisoma kwa udhamini wa utawala wa Kaunti hiyo.

Mkurugenzi wa chuo hicho ameonyesha imani kubwa kwamba, wanafunzi hao watakuwa wa msaada sana katika kaunti zao kwa maswala ya kiteknolojia.

Aliwahimiza kwamba si vyema kungoja kazi za kuajiriwa, bali wanaweza kufanya miradi yao itakayowapa mapato.

Huku hayo yakijiri, Spika wa Kaunti wa Uasin Gishu Hosea Lamai amesema wajumbe katika bunge hilo wamepitisha mswada wa kuipa elimu kitita cha milioni tisini, huku kila wadi ikopokea shilingi milioni tatu, ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha elimu.

Ikiwa mradi huu utafaulu, basi wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kulipa karo watafaidika.