Jamii katika eneo la Pwani inalaumiwa kwa kutochukua hatua kali za kukabili visa vya ubakaji na dhulma dhidi ya watoto.

Share news tips with us here at Hivisasa

Siku ya Jumatano, katibu wa wizara ya leba Susan Momache alisema visa vya dhulma dhidi ya watoto vimeongezeka, na kuitaka jamii kushirikiana na idara husika za kiserikali ili kuomesha visa hivyo.

Alitilia mfano kuwa visa vya ubakaji dhidi ya watoto vimekithiri eneo la Pwani kila uchao na hakuna hatua yoyote ya kuvikabili.

Momache amesema ili kukabili visa hivyo, ni sharti jamii ijitolee kwa kuwaripoti wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Aidha, alizitaka mahakama kutowaachilia washukiwa wa ubakaji bali kuwachukulia hatua kali za kisheria.