Share news tips with us here at Hivisasa

Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu Abdi Hassan amesema kuwa uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa wa moto katika kampuni ya mbao ya Raiply mjini Eldoret umeanzishwa.

Kamishna huyo alisema kuwa moto huo uliozuka usiku wa kuamkia leo (Jumatano), umeharibu mali ya dhamana isiyojulika na wanajaribu kila wawezalo kuudhibiti.

"Tumejaribu kuudhiti moto huu kwa kiwango fulani lakini uhudi bado zinaendelea,” alisema Hassan.

Hassan aidha alisema kuwa ukosefu wa maji ya kutosha na upepo mkali unatatiza shughuli hiyo.

"Mkasa huu umetupa changamoto kama kaunti tuweze kujipanga vizuri ili kukabiliana na mikisa ya baadae,” alisema Hassan.

Hassan alishukuru wafanyikazi wa makampuni waliojitolea kuuzima moto huo, huku akiongezea kuwa hakuna majeruhi ambao wameripotiwa.