Serikali ya kaunti ya Nakuru sasa imepiga marufuku kuuzwa kwa samaki kando ya  barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kupitia kwa idara ya uvuvi, serikali hiyo inasema kuwa uchuuzi huo wa samaki barabarani hususani mjini Naivasha, huenda ukachangia pakubwa kuongezeka kwa ugonjwa wa kipindu pindu.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, vijana wamekuwa wakisimama kando ya barabara hiyo na kuuza samaki kama na njia moja ya kubuni ajira.

Afisa msimamizi wa maswala ua uvuvi eneo hilo Nicholas Kagundu alisema: “hakuna mfanyibiashara hata mmoja aliyepewa leseni ya kuuza samaki kando ya barabara”.

Aidha amesema kuwa idara yake pamoja na mashirika mengine ya kiserikali itafanya msako wakati wowote ili kuwanasa wale wote wanaochuuza samaki barabarani.