Ugomvi uliozuka baina ya bibi na mmewe umepelekea kifo cha ghafla cha mwanao wa umri wa miaka mitatu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni katika eneo la Shonda, kaunti ndogo ya Likoni. 

Amir Ogada ambaye ni jirani ya wazazi wa mtoto marehemu amesema kwamba alisikia kelele na mabishano kuhusu pesa za matumizi na basi hakutaka kuingilia mambo ya kifamilia. 

Mamake Abdul ambaye ni mchuzi wa maji katika ploti hiyo ameongeza kuwa baada ya mume wa mama huyo ambaye pia ni mja mzito kuondoka, alionekana akiwa na wasiwasi mwingi. 

Hapo ndipo jirani alipokuja kwangu mbio huku akisema mtoto wake hapumui baada ya kumwadhibu kwa hasira za mumewe.

Wakazi wa eneo hilo wameshangazwa na kisa hicho na kuwataka wazazi kuwajibika na kupunguza jazba haswa wanapokuwa na watoto wao. Mwanamke huyo ametiwa nguvuni ili kusaidia maafisa wa usalama katika kutoa maelezo.