Wakaazi wa eneo la Ngacura, Bahati viungani mwa mji wa Nakuru wamelalamikia uhaba wa maji katika eneo hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongea na wanahabari mjini Nakuru, wakaazi hao wamedokeza kuwa uhaba huo umekuwepo sasa kwa muda mrefu, hali ambayo inawalazimu kutembea umbali wa kilomita kadhaa kutafuta bidhaa hizo muhimu.

Kwa mujibu wa Paul Wangai na ambaye ni mwenyekiti wa Ndeffo Community Water Project, amehoji  kuwa jitihada za wakaazi hao za mara kwa mara za kutafuta mbinu za kupata maji ya kudumu zinaambulia patupu huku wakisalia na ahadi zisizotimizika.

Aidha wamedokeza kuwa zoezi la kununua maji kila kuchao inagharimu hela nyingi ikizingatiwa kuwa wengi wa wakaazi katika eneo hilo wanaishi katika maisha duni.

Kwa sasa wameitaka  serikali ya jimbo la Nakuru kupitia kwa uongozi wake Gavana Kinuthia Mbugua kuwakumbuka kwa kutafuta suluhu la kudumu kwa janga hilo linalowakumba.