Wakaazi mjini Molo wanaendelea kulalamikia uhaba wa maji huku wakiitaka kampuni ya kusambaza maji Nakuru Water and Sanitation Company (Nawassco) kutekeleza majumu yake ipasavyo ili waweze kupata bidhaa hiyo muhimu.
Wakazi hao wamesema tangu mwezi Desemba mifereji yao imekuwa na kiu cha maji safi licha ya wao kuendelea kutozwa ada za maji na kampuni husika.
Wamesema wamekuwa wakitumia maji kutoka kwa mito iliyoko nje ya mji huo kama njia mmoja ya kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Wakazi hao wamesema wanahofia huenda maji wanayoteka kutoka mito hiyo ikawa na viini ambayo huenda vikasababisha mkurupuko wa maradhi yanayochangiwa na matumizi ya maji chafu.
Ukosefu huo umesabisha ushindani mkubwa wa bidhaa hiyo huku wachuuzi wa maji wakieleza kuimarika kwa biashara yao hasa mwezi huu wa Januari ambapo kiangazi kimeshamiri.
Moses Kuria ambaye ni mkaazi wa mji huo amesema wananchi wanalazimika kutembea mwendo mrefu ili kupata maji.
Wamiliki wa biashara ikiwemo hoteli wamesema uhaba huo umeadhiri biashara zao huku wakilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka kwa wachuuzi wanaoteka maji mitoni.
Wakazi hao wamesema baadhi ya mito inayotegemewa inaendelea kukauka huku wakiitaka kampuni ya kusambaza maji kutakua hali hiyo.