Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa soko la Kongowea kuwa ardhi inayodaiwa kunyakuliwa na mabwanyenye itasalia kuwa ya soko hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yanajiri baada ya kamati ya maslahi ya wafanyabiashara wa soko la hilo kutaka swala hilo la unyakuzi wa ardhi kuangaziwa.

Musyoka Mutie, mwenyekiti wa kamati hilo, amedai kuwa kuna baadhi ya wanasiasa kutoka Pwani ambao wanataka kumiliki jengo jipya ambalo lilifunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta.

Mutie alisema kuwa kabla ya kukarabatiwa kwa soko hilo, kulikuwa na baadhi ya maduka ambayo yalikuwa tayari yamenyakuliwa na wanasiasa.

Kwa upande wake, Rais Uhuru ameitaka kamati hiyo kuwa macho na kupiga ripoti pindi tu watakapohisi kunyanyaswa na baadhi ya viongozi wanaotumia nyadhifa zao kiimla.

Uhuru yuko kwenye ziara ya siku tatu katika eneo la Pwani, anapotarajiwa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.