Rais Uhuru Kenyatta, amewaonya vijana katika kaunti ya Kisumu dhidi ya kukubali kutumiwa na wanasiasa. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia wananchi mjini Kisumu, Kenyatta alisema kuwa taifa hili linahitaji nguvu za vijana katika kuafikia maendeleo yake.

“Maendeleo haita-afikiwa, iwapo sisi kama wakenya tutakubali kugawanywa kwa misingi ya siasa, dini na kabila,” akasema Kenyatta.

Kenyatta pia aligusia suala la usalama akisema kuwa serikali yake iko imara kukabiliana na magaidi na ugaidi.

Raisi pia alisema kuwa kila mkenya ana jukumu la kushirikiana na serikali kufanikisha vita dhidi ya ugaidi.

Mamia ya wananchi walijitokeza jijini Kisumu kuona msafara wa rais Kenyatta, na ikambidi kiongozi huyo kuwahutubia.

Alikuwa akitoka katika chuo cha Leba cha Tom Mboya, kuelekea katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kisumu.

Kenyatta alikuwa ameitembelea kaunti ya Kisumu kufungua rasmi kongomano la pili la magavana linaloendelea katika kaunti hiyo.

Katika ziara yake raisi alizindua mradi wa ujenzi wa mtaa wa mabanda wa Nyalenda.