Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wafanyabiashara katika Kaunti ya Mombasa kujiunga na vyama vya akiba na mikopo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Rais Kenyatta alisema kuwa hatua huyo ni njia mojawapo ya kupanua na kuendeleza biashara katika masoko mbalimbali eneo la Pwani.

Akihutubia wakaazi na wafanyabiashara katika soko la Kongowea kwenye hafla ya ufunguzi wa soko hilo siku ya Jumanne, Rais Kenyatta alisema hiyo ndiyo njia pekee ya kujinasua kutoka wimbi la umaskini ambalo linazidi kutajwa kama janga kubwa Pwani.

Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na wajumbe mbalimbali ikiwemo viongozi wa Kaunti ya Mombasa, alisema kuwa vyama hivyo vitawawezesha wafanyabiashara kujiendeleza kimaisha.

Aidha, rais alisema kuwa serikali inatambua masaibu wafanyabiashara wa soko hilo wanayopitia, na kwamba serikali iko katika mchakato wa kurekebisha barabara zote zinazoingia na kutoka kwenye soko hilo, ili kurahisisha shughuli ya kusafirisha mizigo.

Hata hivyo, ameitaka serikali ya Kaunti ya Mombasa kushirikiana na serikali kuu ili kuboresha mazingira ya soko hilo.