Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Molo kwenda Olenguruone Jumatano hii kwenye kituo cha kibiashara cha Moto.
Barabara hio ambayo imekua katika hali mbaya kwa miaka mingi ni mojawapo wa azimio la serikali ya Jubilee ya kukarabati kilomita 10,000 za barabara kama walivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2013.
Zabuni ya kuunda barabara hii ilitunukiwa kampuni ya ujenzi barabara ya kichina ambayo tayari ishaanza kazi hio.
Viongozi wa eneo hili na maafisa wakuu serikalini wataandamana na Rais kwenye hafla hii.