Balozi wa uingereza nchini Nic Hailey amesema kuwa uingereza inashirikiana na serikali ya Kenya katika vita dhidi ya ugaidi ili kuhakikisha kuwa vita hivyo vimemalizika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na wandishi wa habari baada ya kukutana na mshirikishi wa kanda za Pwani Nelson Marwa katika afisi yake ya Uhuru na Kazi, bwana Hailey alisema kuwa iwapo ugaidi utakithiri humu nchini basi hata uingereza utaathirika kwa kuwa nchi hizo mbili hufanya biashara ya pamoja.

“Tishio la ugaidi na vijana kuungana na makundi yenye itikadi kali si geni hata kwa nchi ya uingereza, mbali yataka ushirikiano ili kuhakikisha kuwa imemalizika kabisa,” alisema balozi Hailey.

Uingereza imejitosa katika kutoa msaada wa kifedha, vifaa vya vita na mafunzo ya kivita ambayo hutekelezwa katika kambi ya majeshi wa uingereza ya Naivasha ili kuhakikisha kuwa imemaliza ugaidi humu nchini.