Takiriban Vijana 600 katika kaunti ya Mombasa wamenufaika na ufadhili wa shilingi milioni 100 kutoka kwa serikali ya Uingereza kwenye mradi wa Kuza ambao huwasaidia vijana wanaoshindwa kukamilisha masomo yao ili kupata mbinu za kujikimu kimaisha.
Kwa mujibu wa Balozi wa Uingereza nchini Kenya Nick Heiley, ufadhili huo utasaidia pakubwa vijana hao kupata masomo ya kiufundi na biashara kama njia moja wapo ya kijitafutia maisha.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano katika hafla hiyo, Heiley alisema kuwa serikali ya Uingereza inashirikiana kwa karibu mno na serikali ya Kenya kuhakikisha kuwa vijana wanapata elimu itakayowawezesha kuwafanikisha ndoto zao maishani.
"Ufadhili tumetoa kutoka kwa serikali ya Uingereza umeonyesha ushirikiano mwema baina ya Kenya na Uingereza na tunawaomba mtumie fursa hiyo kufanikisha malengo yenu, na lazima tutahakikishe tunazidi kusaidiana," alisema Heiley.
Mradi huu wa Kuza unalenga kuwasaidia vijana katika kaunti ya Mombasa kuhakikisha kuwa wanapata masomo dhabiti ya kuwawezesha kuweza kujiajiri wenyewe na kukimu maisha ya familia zao.
Picha: Balozi wa Uingereza nchini Kenya Nick Heiley. Amewahimiza vijana kutumia fursa ufadhili uliotolewa na serikali ya Uingireza kuendeleza masomo yao kujikimu kimaisha.