Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bandari nchini KPA, Marsden Madoka, amesema kuwa huenda ujenzi wa bandari ya Lamu ukachukua muda zaidi kabla ya kukamilika.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Madoka alisema kuwa mradi huo unahitaji kima cha shilingi bilioni 42 kukamilika, fedha ambazo haziwezi kutengwa kwa sasa hadi serikali itakapokamilisha mipangilio yake.

Akizungumza afisini mwake bandarini Mombasa siku ya Ijumaa, Madoka alisema kwamba fedha zaidi zinahitajika kujenga milango mitatu itakayotumika katika bandari hiyo.

“Kwa sasa bandari hiyo itasubiri kwa muda kutokana na kuwa serikali ina mipango mingi muhimu na fedha zinazohitajika ni nyingi mno. Tunahitaji zaidi ya shilingi bilioni 42 na kufikia sasa serikali imefanikiwa kutoa shilingi bilioni tano pekee,” alisema Madoko.

Mradi huo unatarajiwa kutoa nafasi za ajira kwa zaidi ya vijana 1,000.