Wakazi wa eneo la Chabera na Ikonge wana kila sababu ya kutabasamu huku ukarabati wa barabara kuu ya Ikonge hadi Chabera ikiendelea kukarabatiwa.
Ujenzi wa barabara hiyo ulianza mwezi wa Agosti mwaka jana, na umeendelea vizuri huku barabara hiyo ikitarajiwa kuwasaidia wengi wa wakazi.
Hata hivyo, mbunge wa eneo hilo la Mugirango kaskazini Charles Geni alipotembelea eneo hilo aliwahakikisia wakazi wa eneo hilo kuwa barabara hiyo itakamilishwa kwa muda wa mwaka mmoja ujao.
Mbunge huyo vilevile aliwaonya watakaokuwa wakitumia barabara hiyo wafuate sheria na kanuni za barabara ili kuepukana na ajali nyingi za barabara.
Wakazi wa eneo hilo wamepata faida ya kuajiriwa na kampuni hiyo inayokarabati barabara hiyo na vile vile biashara zinaendelea kukua katika sehemu hiyo.